Waridi lisilo miba (Rose without thorns)

Lyrics and translation
Ewe kiumbe wa shani nalipenda umbo lako
Oh you marvellous creature I love your shape
Mzuri uso kifani kakuumba Mola wako (2)
Beautiful with no equal your Lord created you
Katu humu duniani hapana mfano wako (2)
Nowhere in this world is there anyone like you

Kiitikio (Refrain)

Ewe ua la peponi
Oh you flower of paradise
Waridi lisilo miba
Rose without torns
Kwenu kakutoa nani kwenye maskani yako
Who tore you from your place
Bilisi au Shetani kakuiba kwa wenzako (2)
The devil or a demon stole among your companions
Mabanati wa peponi hao ndio fani yako (2)
The girls of paradise you are just like them
Ewe ua la peponi
Oh you flower of paradise
Waridi lisilo miba
Rose without torns
Nani atakuthamini akijue cheo chako
Who will respect you recognizing your position
Nani atakuzabuni alipe thamani yako (2)
Who will appraise you compensating your value
Naapa ulimwenguni simdhani kama yuko (2)
I swear in this world I don’t think he exists
Ewe ua la peponi
Oh you flower of paradise
Waridi lisilo miba
Rose without torns
Naipotea imani kifikiri tabu yako
I lose confidence when I think about the problems with you
Huingiwa na huzuni kikumbuka pendo lako
It makes me sad when I remember your love
Naingiwa na imani kifikiri tabu yako
I get more confident when I think about the problems with you
Naingiwa na huzuni kikumbuka pendo lako
It makes me sad when I remember your love
Kama utaniamini nifanye ni mlezi wako (2)
If you believe me please make me your custodian